MASTAA wetu Bongo ukimtokea ghafla na ukataka kumpiga picha bila kujiremba unaweza kumuua kwa hofu, siku za karibuni kamera ya FC ilimkosesha raha nyota wa filamu Swahiliwood Kajala Masanja pale alipokutana na mpiga picha wetu na kutaka kumpiga picha kama sehemu ya kumbukumbu katika matukio, msanii huyo alizuia huku akilalamika.
.
.
“Aaah sitaki jamanii unanipigaji picha hivi hata sijajiandaa jamani, nipo rafu sipendi ukipiga picha angalau uwe smart, usinipige picha sitaki sitaki sijajiandaa picha zitakuwa mbaya please usifanye hivyo,”anasema.
Utafiti unaonyesha kuwa mara nyingi nyota wa filamu wamejenga tabia ya kujiandaa kwa kujipodoa wakiwa wapo location au wakifanya mahojiano na wanahabari, hivyo kuwa na muonekano tofauti na wanavyokuwa na maisha ya kawaida wakiwa katika mishemishe za maisha halisi.
CHANZO: Filamu Central
No comments:
Post a Comment