Saturday 5 October 2013

MASHINDANO YA BIBI BOMBA BI.MGENI AIBUKA KIDEDEA

NA JELARD LUCAS(GLP)
MASHINDANO ya Bibi Bomba yamemalizika usiku wa kuamkia leo na ambapo Bi.Mgeni Ibrahimu ameibuka kidedea na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 12
Tukio hilo limefanyika maeneo ya Ukumbi wa Complex Mikocheni na Mshindi wa Pili ni Veronica Kayombo alijinyakulia kitita cha Shilingi 500,000/= akifatiwa na Mshindi wa tatu Tabitha Tungalaja nae alipokea bahasha ya shilingi 300,000/= , kuhudhuriwa na watu mbalimbali pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Dar, Bi.Masaburi Mke wa Meya wa jiji la Dar, alimwakilisha Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mh.Sophia Simba.
Hata baadhi ya washiriki 5 waliobakia wote walitunukiwa vyeti kutoka Kampuni ya Cloudz Media Group kama sehemu ya kutambua uwepo wao na ushiriki wa shindano la Bibi Bomba season 2.
Akiongea na Cloudz Tv Bi.Mgeni alisema amefurahia sana kupokea ushindi huo kwani hakutegemea kama ataibuka mshindi.
“Nafurahia sana kushinda nimepokea kwa furaha ushindi huu kwani sikutegemea kabisa kwani mchakato ulikuwa mgumu” Alisema Bi.Mgeni.
1. Bi.Mgeni Ibrahimu (Katikati) akiwa na Wadhamini wa Shindano la Bibi Bomba kutoka kampuni ya ‘Wazazi Nipendeni’ iliyo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii’.
2. Baadhi ya top 5 ya Bi.Bomba kabla ya kupatikana Mshindi
3. Mtangazaji (katikati) Babu wa Kitaa akiongea na Bi.Mgeni kabla ya kutangazwa Mshindi, kulia ni Bi.Veronica Kayombo
4. Bi.Mgeni akifanya manjonjo yake mara baada ya kutangazwa Mshindi.
CHANZO: GPL

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...