Saturday 5 October 2013

MFAHAMU ALEK WEK, MREMBO KUTOKA SUDANI YA KUSINI



File:Alek Wek, Red Dress Collection 2007.jpg     

  
Alek Wek ni mrembo raia wa Uingereza mwenye asili ya  Sudani ya kusini.Asili yake ni kabila la Dinka.
Alek alizaliwa mwaka 1977. Kwa mujibu wa mama yake,jina lale "ALEK" linamaanisha "Ngo'mbe yenye madoadoa meusi.
 Mwaka 1991 yeye na mdogo wake wa kike  walikimbilia Uingereza kuungana na dada yao mkubwa aliyekuwa tayari akiishi nchini humo kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi yao(Sudani ya Kusini).Akiwa Uingereza alifanyakazi mbalimbali baada ya shule na kutuma pesa kwa mama yake aliyebakia Sudani ya kusini.Mama yake na nduguze wengine wawili kati ya tisa walihamia Uingereza baada ya miaka miwili. Nduguze wengine waliobakia  walipewa hifadhi ya kikimbizi nchini Kanada na Australia.
Alek alijifunza Kingereza haraka na kusomea mitindo na biashara katika Chuo cha Mitindo London.
Kipaji chake cha uana mitindo kiliibuliwa mwaka 1995 ambapo alisaini mkataba na Model 1.
Baadaye alihamia Marekani.
Miongoni mwa mambo mengine amefanya matangazo ya Issey Miyake, Moschino, Victoria's Secret na kampuni ya manukato Cliniquena vile vile alionyesha mtindo ya wabunifu wakubwa kama Yohana Galliano, Donna Karan, Calvin Klein na Ermanno Scervino. Mwaka wa 2002 alishiriki katika uigizaji mara ya kwanza katika filamu iitwayoThe Four Feathers kama malkia Aquol wa Sudan.
WEK pia amebuni mitindo mbalimbali ya mikoba inayoitwa "WEK 1933", ambayo inapatikana katika maduka kadhaa yaliyochaguliwa . Mwaka "1933" ni mwaka  ambao baba yake alizaliwa.
Yeye ni mjumbe wa Kamati ya Marekani ya Wakimbizi( US Committee For Refugees' Advisory Council) na kwa kutumia uzoefu wake kama mkimbizi,anasaidia kuongeza ufahamu kuhusu hali nchini Sudan, vile vile hatma ya wakimbizi duniani. 
PICHA ZAIDI za Alek bofya READ MORE
Alek akiwa na mbunifu Karl Lagerfeld



No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...