Sunday 6 October 2013

NIMEANZA KAZI KWA KASI KUBWA-STARA

Wastara Juma
Wastara mwigizaji wa filamu Swahiliwood.
MSANII wa kike katika tasnia ya filamu Bongo Wastara Juma ‘Stara’
amesema ameingia kazini kwa nguvu katika hali ya kukabiliana na hali
halisi ya maisha kwani anahitaji kuhudumia familia yake pasipo
kumtegemea mtu maana aliyekuwa akimsaidia hayupo tena, anasema
kuwa awali alikuwa katika mapumziko falme za Kiarabu Dubai toka
arudi anafanya kazi kwa nguvu.

.
Wastara Juma
Stara akiwa katika pozi lake.
Wastara Juma 604 B
Wastara Juma, Yusuf Mlela
Stara akiwa na Yusuf Mlela katika moja ya filamu mpya.
“Nimekusudia kufanya kazi kwa nguvu ili kuwasaidia wanangu
maisha ya sasa si ya kuwa tegemezi, namshukru mwenyemungu
watayarishaji wenzangu wananikumbuka katika kazi zao wananihita
na kunipa nafasi ya kushiriki katika filamu zao na kunilipa vizuri, na nimejipangia kufanya hivyo na kuandaa kazi zangu kujikwamua
kimaisha si unajua mimi ndio kila kitu kwa sasa,”anasema Stara.


Stara hadi sasa tayari amerekodi filamu tano ambazo bado kutoka na
kuingia sokoni , msanii huyo alisimama kufanya kazi baada ya
kuuguliwa na marehemu mume wake marehemu Sajuki baada ya kifo
cha mumewe aliondoka na kusafiri kwenda Uarabuni kwa ajili ya
mapumziko, hali hiyo ilitokana na utendaji wa kazi wake na
marehemu katika kampuni yao ya Wajey film hivyo alihitaji
kupumzika kabla ya kuanza kufanya kazi akiwa pekee yake.
CHANZO: FILAMU CENTRAL

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...