Thursday, 10 October 2013

USIKOSE MDAU: P-SQUARE KUTUA BONGO NOV- 23-2013‏

   Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasilino wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa, akisisitiza jambo  kwa waandishi wa habari wakati wa kutangaza ujio wa wasanii wa Muziki wa kizazi kipya Peter na Paul  Okoye maarufu kama  P – square  kutoka nchini Nigeria chini ya udhamini wa Vodacom  Tarehe 23 Mwezi ujao. Wasanii hao wataambatana na wasanii wengine 13 kutoka nchini humo. Pamoja nae katika picha ni Mtangazaji wa East Afrika Radio, Hillary Daudi (Zembwela).
Mkuu wa Idara ya  Masoko na Mawasilino wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza ujio wa wasanii wa Muziki wa kizazi kipya Peter na Paul Okoye maarufu kama  P – square  kutoka nchini Nigeria chini ya udhamini wa Vodacom, watakaowasili Tarehe 23 Mwezi ujao. Wasanii hao wataambatana na wasanii wengine 13 kutoka nchini humo. Pamoja nae katika picha ni Mtangazaji wa East Afrika Radio, Hillary Daudi (Zembwela).
Mtangazaji wa East Afrika Radio, Hillary Daudi (Zembwela)akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza ujio wa wasanii wa muziki wa kizazi kipya Peter na Paul Okoye maarufu kama  P – Square  kutoka nchini Nigeria pamoja na mdhamini Mkuu,Tarehe 23 Mwezi ujao ndipo watawasili nchini. Wasanii hao wataambatana na wasanii wengine 13 kutoka nchini humo. Pamoja nae katika Picha ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasilino wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa ambo ndio wadhamini wa onesho hilo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa wazungumzaji Mtangazaji wa East Afrika Radio, Hillary Daudi (Zembwela).  Na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasilino wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa , wakati wa Kutangaza  ujio wa wasanii wa Muziki wa kizazi kipya Peter na Paul Okoye maarufu kama  P – square  kutoka nchini Nigeria,  Tarehe 23 Mwezi ujao. Wasanii hao wataambatana na wasanii wengine 13 kutoka nchini humo.
Dar es Salaam 10  Oktoba 2013 …… Kama ni siku ambayo inasubiriwa kwa hamu na wapenzi wa muziki basi ni Novemba 23 ambapo wasanii Mapacha Petter na Paul Okoye,wanaojulikana kama “P – Square” watatoa burudani ya karne katika viwanja vya leaders Club jijini Dar es Salaam chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania.
Wasanii hao kutoka nchini Nigeria kwa sasa wanatamba na kibao chao cha Personally wameendelea kukonga nyoyo za wapenda burudani ndani na nje ya bara la Afrika huku matamasha yao yakivutia mamia ya mashabiki na kupata mapokezi makubwa kila wanafanya tamasha.


Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt jijini Dar, Hillary Daudi wa East Afrika Radio, Amesema onesho hilo litakuwa la kipekee. P- Square wataongozana na wasanii wengine 13 ambao watatoa burudani ya Live Band siku hiyo. Pamoja na wasanii wengine kutoka Tanzania.
“Wote tunatambua namna kundi hili linavyofanya vizuri ndani na nje ya bara la Afrika, licha ya kutoa burudani kwa mashabiki, pia litatoa fursa kwa wasanii wa ndani kujifunza kutoka kwa wasanii hawa vijana ambao wamepata mafanikio makubwa kutokana na kazi yao ya muziki,” alisema na kuongeza “hii itakuwa ni fursa ya kipekee kwa wasanii wetu wa bongo kujifunza kwa kuangalia wenzao wanavyofanya kazi”.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, ambao ndio wadhamini wakuu wa onesho hilo  amesema Vodacom inafurahi kuendelea kuwa sehemu ya kutoa burudani kwa jamii ya Watanzania na safari hii ikiwaleta wasanii ambao ni kipenzi cha Watanzania wengi.
“Siku zote Vodacom imeendelea kuwa chaguo la kwanza kwa Watanzania, kuanzia katika burudani na hata huduma nyingine za mawasiliano na kijamii. Tunaendelea kuunga jitihada za kuwainua wasanii wetu wa ndani kwa kuwapatia fursa ya kujifunza kutoka kwa wasanii wenzao  wakubwa waliofanyikiwa kufanya kazi zao Kimataifa.” Alisema Twissa na kuongeza
“Kwa wateja wa Vodacom ambao pia ni mashabiki wa wasanii hawa ambao wanatamba na kibao chao kitamu cha ‘Personally’ kwa sasa wanayo fursa ya kufurahia nyimbo hizi kwa kuzidownload au kuzitumia kama miito ya simu (RBT) na kuweza kujishindia tiketi za onesho hilo. Natoa wito kwa Watanzania wapenda burudani kutembelea ukurasa wetu wa Facebook na Twitter kwa taarifa zaidi na kujua namna ya kujishindia tiketi za onesho hilo.
Tamasha hilo linalo ratibiwa na East Afrika Radio na TV na kudhaminiwa na kampuni ya Vodacom Tanzania Linatarajiwa kuwa la kihistoria katika burudani  ya muziki wa kizazi kipya nchini.
CHANZO: GPL

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...