Kama kuna nchi imejaliwa kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii basi ni Tanzania. Nadhani tuna hifadhi za taifa katika pande zote nne za nchi yetu!Je,tunazitumia kama inavyostahili?Hakika huu ni utajiri mkubwa mno kwani ni sawa na mtu kutokuwa na chochote halafu ukapewa kipande kikubwa cha almasi na kuambiwa haya,nenda kaanze maisha!Kwa kuwa na kipande hicho cha almasi tayari wewe ni tajiri kama utajua jinsi gani almasi hiyo itaongoza maisha yako.Ukidanganyika au kutokuwa na mikakati mizuri basi utapoteza almasi hiyo na kuendelea na umaskini wako.Kumbuka kuwa ulipopewa kipande cha almasi kuna waliokuona hivyo wakiona kuwa wewe bado ni masikini watakushangaa na kukudharau kwamba "yaani huyu amepewa kipande cha almasi amekifanyia nini? Mbona bado anaishi maisha yaleyale tu".
Mbwa mwitu katika hifadhi za Mkomazi
Vifaru katika hifadhi za Mkomazi.
Ndege katika hifadhi za Mkomazi.
Hifadhi za Mkomazi.
Hifadhi ya Mkomazi inatokana na muungano wa Umba Game Reserve iliyopo katika wilaya ya Lushoto mkoani Tanga na Mkomazi Game Reservekatika wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.
Wanyama wanaopatikana katika hifadhi za Mkomazi ni Faru, mbwa mwitu,twiga, pundamilia, tembo.
Kipindi kizuri cha kuona wanyama na ndege ni kuanzia mwishoni mwa mwezi juni mpaka Septemba. Na kwa kuona uoto mzuri ni kati ya mwezi ya machi na juni.
Imeandikwa na Anna Nindi
No comments:
Post a Comment