Kamati ya ulinzi na usalama wilayani Mkinga imebaini kuwepo kwa kisiwa maalum cha maficho ya wahamiaji haramu kutoka Somalia na Ethiopia ambapo wametengeneza kiwanja maalum ndani ya kisiwa hicho kwa ajili ya kufanya mazoezi.
Kisiwa hicho kinachojulikana kwa jina la Kirui chenye ukubwa wa hekta 600 kilichopo katika bahari ya hindi kimeanza kuleta hofu kwa Kamati hiyo ambapo askari waliokuwa na silaha mbali mbali walilazimika kuvamia kisiwa hicho kwa muda wa siku mbili na kufanikiwa Kukamata wahamiaji haramu kutoka Ethiopia na Somalia wapatao 22 huku wengine wakidaiwa kutoroka ndani ya kichaka cha msitu huo wa miti aina ya mikoko.
Kwa upande wake afisa misitu wilayani Mkinga bwana Frank Chambo amesema akielezea uharibifu uliofanywa na baadhi ya watu Kutoka nchini Kenya amesema wamebaini kuwepo kwa shehena ya magogo pamoja na mbao baada ya kuazisha viwanda vidogo ndani ya hifadhi hiyo.
Kufuatia hatua hiyo afisa uhamiaji mkoani Tanga bwana Sixtus nyaki amesema idara yake imeanza kufanya utaratibu wa kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kutumikia kifungo kisha kuwarejesha nchini mwao lakini taarifa walizonazo lipo kundi kubwa la wahamiaji kutoka nchi mbali mbali na hivi sasa wanaandaa utaratibu ili kuvamia ndani ya pori hilo.
CHANZO; ITV
No comments:
Post a Comment