Wasanii wakali kabisa Afrika, P Square hatimaye wamedondoka ndani ya jiji la dar kwa Kishindo kikubwa tayari kwa mashambulizi juu ya jukwaa siku ya jumamosi pale Leaders Club Kinondoni jijini Dar.
Wasanii hawa wameambatana na timu kubwa kabisa ya wasanii walio nyuma yao kwaajili ya kukamilisha mzigo wa live band ambao utatikisa jiji siku ya onyesho.
Wasanii hawa wamesema kuwa, wamefurahi sana kuja kutoa burudani hii Bongo ikiwa ni mara yao ya pili baada ya miaka mitano sasa, na wamewataka watanzania kuongea yote baada ya kushuhudia show ambayo itatafsiri maana halisi ya burudani juu ya jukwaa siku ya Jumamosi bila kukosa.
CHANZO: EATV
No comments:
Post a Comment