Picha na Aftonbladet
Zaidi ya watu 10,000 wameandamana leo katika eneo la Kärrtorp kusini mwa jiji la Stockholm, Sweden kupinga ubaguzi.
Maandamano ya leo yamefanyika baada ya vurugu zilizofanywa na kundi lenye mlengo wa kibaguzi jumapili iliyopita tarehe 15 disemba.
Mbali na kufanyika kwa maandamano hayo ya kupinga ubaguzi leo jijini Stockholm, baadhi ya miji mingine nayo imeunga mkono jitihada hizo kwa kuandaa maandamano kama hayo leo hii. Miji hiyo ni kama Borås, Luleå, Malmö , Motala na Östersund.
Mbali na wananchi wa kawaida baadhi ya mawaziri wa serikali inaoongoza na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa vya Sweden nao walikuwepo.Mmoja wapo ni Stefan Löfven wa chama cha social demokrat ambacho ni chama kikubwa cha upinzani.
Uwepo wa viongozi hao ilikuwa ni kuonyesha kuunga mkono upingaji ubaguzi wa aina mbalimbali nchini Sweden.
Pia kulikuwa na ulinzi mkali wa polisi wakiwa na magari mbalimbali, mbwa na helikopta
Gari ya polisi ikilinda amani katika shopping square ya Kärrtorp,eneo yalikoanzia maandamano hayo.
Baadhi ya waandamanaji wakitoka katika maandamano hayo
Picha kwa hisani ya kamera ya rainbow -tz blog,Stockholm,Sweden
No comments:
Post a Comment