Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Halima Dendegu
Serikali mkoani Tanga, imesema tafiti mbalimbali zilizofanyika kwa kuwashirikisha watafiti wa kimataifa zimebaini kuwapo kwa mafuta na gesi asilia kwenye vijiji mbalimbali vilivyopo katika ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi.
Nishati hizo zimebainika kuwapo katika wilaya za Tanga, Pangani na Mkinga na kwamba serikali kwa kushirikiana na watafiti hao wanaendelea na mchakato kufahamu kiasi kilichopo tayari kuanza kufanya majaribio ya rasilimali hiyo.
Akizungumza katika mahojiano na NIPASHE muda mfupi baada ya kufungua warsha ya wanahabari pamoja na asasi za kiraia kuhusu uzuruaji wa mafuta na gesi asilia iliyoandaliwa na Shirika la Kimataifa linalojihusisha na Hifadhi Mazingira (WWF), Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendegu, alisema hatua hiyo ni mojawapo ya fursa za kiuchumi mkoani humu.
Dendego aliyataja maeneo ambayo hivi sasa yanafanyiwa utafiti na wataalam wa kimataifa kwa kutumia meli katika ukanda wa Bahari ya Hindi kuwa ni vijiji vya Marungu na Tongoni kwa upande wa Jiji la Tanga.
Akizungumzia hatua hiyo, Meneja Uhifadhi wa WWF, Gerad Kamwenda, alisema lengo hasa la kuwahusisha wanahabari katika mafunzo hayo ni kutokana na kutokuwa na usahihi wa habari zinazoandikwa kuhusu kuwapo kwa gesi na mafuta kwenye maeneo mbalimbali nchini na kwamba nyingi hazifanyiwi utafiti wa kina.
CHANZO: NIPASHE
|
Wednesday, 18 December 2013
MAFUTA, GESI ASILIA VYAGUNDULIKA TANGA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
PALM TREES ARE BEAUTIFUL
Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...
-
Dar es Salaam: Mwekezaji Sheikh Salim Abdullah ametangaza kuwekeza kwenye Uwanja Wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere Dar es Salaam (JN...
-
1. PASTA Hiki ni chakula cha haraka.Unaweza kutayarisha pasta kwa kuongeza tu protini ulizonazo katika jokofu lako mfano kuku...
No comments:
Post a Comment