Wednesday 11 December 2013

MWILI WA RAIS WA KWANZA MWEUSI WA AFRIKA YA KUSINI NELSON ROLIHLAHLA MANDELA WAWASILI KATIKA MAJENGO YA UMOJA PRETORIA KWAAJILI YA UMMA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO

Jeneza lililobeba mwili wa rais wa kwanza mweusi wa Afrika ya kusini,Nelson Rolihlahla Mandela likiwa ndani ya gari kuelekea katika majengo a Umoja,mjini Pretoria
Pall bearers carry Nelson Mandela's casket into the Union Buildings in Pretoria
Mwili wa Nelson Mandela ukiingizwa katika majengo ya umoja mjini Pretoria, Afrika ya kusini

Mwili wa aliyekuwa rais wa Afrika ya kusini Nelson Mandela umewasili katika majengo umoja ya mjini Pretoria tayari kwa umma kutoa heshima za mwisho.
Msafara wake ukitokea hospitali ya jeshi ambapo uliihifadhiwa uliongozwa na pikipiki huku jeneza lililobeba mwili wake likiwa  limefunikwa na bendera ya taifa la Afrika ya kusini.
Ikumbukwe kuwa majengo haya ndipo zilipokuwa ofisi za mzee Mandela baada ya kuapishwa kwake kama rais wa kwanza mweusi wa Afrika ya kusini mwaka 1994.Hata rais wa sasa ameendelea kutumia majengo hayo kama ofisi zake.
Baadhi ya wakazi wa Pretoria wamejitokeza na kujipanga barabara kushuhudia jeneza lililobeba mwili wa Mandela likipitishwa huku wakiimba nyimbo zilizokuwa zikiimbwa wakati wa harakati za ukombozi wa taifa hilo.
Mwili wa Mandela utasafirishwa siku ya Jumamosi kuelekea katika kijiji cha Qunu tayari kwa mazishi siku ya Jumapili.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...