Ndege aina ya Boeing 767-383ER ya shirika la Ethiopian Airline ikiwa imetua kwa dharura kwenye uwanja wa ndege wa Arusha na kuingia pembezoni kwenye njia ya kurukia.
Ndege kubwa ya shirika la Ethiopian Airlines iliyokuwa na abiria 200 imelazimika kutua ghafla kwenye uwanja wa ndege wa Arusha leo mchana muda wa saa saba na robo mchana.
Utuaji huo ulikuwa wa hatari kwakuwa njia ya ndege ya uwanja huo ina urefu wa mita 1.620 ama futi 5.315, urefu ambao ni mdogo mno kwa ndege hiyo ya Boeing 767-383ER kutua.
Kuna taarifa kuwa ndege hiyo ilishindwa kutua KIA kwakuwa kulikuwa na ndege iliyokuwa imeziba njia na hivyo kuamua kwenda Arusha kwakuwa uwezakano wa kwenda kwenye uwanja wa ndege unaomudu ukubwa wake ulikuwa mkubwa kwakuwa ndege hiyo haikuwa na mafuta ya kutosha.
Maswali mengi yameendelea kuulizwa sababu ya rubani wa ndege hiyo kutua ghafla kwenye uwanja huo. Ndege hiyo yenye namba ET-AQW ilikuwa inatokea Addis Ababa kwenda Zanzibar kupitia Kilimanjaro. Hakuna aliyeumia kwenye utuaji huo uliosababisha uwanja wa ndege wa Arusha ufungwe kwa muda.
No comments:
Post a Comment