Thursday 12 December 2013

Sakata la mtafsiri wa lugha ya alama SA

Thamsanqa Dyantyi mtafsiri wa lugha za ishara
 anayelalamikiwa
Serikali ya Afrika Kusini imesema kampuni iliyomtoa mtafsiri wa lugha za ishara wakati wa ibada ya kumbu kumbu kifo cha Nelson Mandela imekuwa akidanganya kwa miaka mingi na imekuwa itoa watafsiri wenye kiwango cha chini.
Wataalamu wa lugha za ishara wamesema mtafsiri huyo wa lugha za ishara, Thamsanqa Dyanty, alikuwa "akitapatapa" wakati wa ibada hiyo siku ya jumanne.

Katika maoni yake mtafsiri huyo anayelalamikiwa, Bwana Dyanty , amesema alipatwa ugonjwa wa kuchanganyikiwa.Naibu Waziri wa Afrika Kusini Hendrietta Bogopane - Zulu amesema hakuna suala lolote la kukiuka taratibu za kiusalama wakati mtafsiri huyo alipokuwa akisimama kwani alikuwa na vibali halali.

Kwa upande wake mmiliki wa kampuni iliyomtoa mtafsiri huyo ametupilia mbali madai ya Naibu waziri Bogopane Zulu.
Awali Naibu Waziri huyo aliwaomba radhi jamii ya viziwi kwa kiwango cha chini cha kutafsiri kilichofanywa na Bwana Dyantyi kutoka kampuni ya SA Interpreters.
"Mtafsiri huyo anazungumza lugha ya Xhosa hivyo kiingereza kulikuwa kigumu sana kwake," alisema Waziri huyo.
CHANZO: BBC

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...