Monday 9 December 2013

Tanzania yatimiza miaka ya Uhuru leo


Tanzania leo inaadhimisha miaka 52 ya uhuru katika sherehe zitakazofanyika kitaifa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Tanzania  leo inaadhimisha miaka 52 ya uhuru katika sherehe zitakazofanyika kitaifa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.



Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu, mgeni rasmi atakuwa Rais Jakaya Kikwete ambaye atakagua gharide la askari wa mvikosi vya ulinzi na usalama.

Aidha, sherehe hizo zitapambwa na halaiki, sarakati, vikundi mbalimbali vya burudani zikiwamo ngoma za asili kutoka katika baadhi ya mikoa ya Tanzania bara na Zanzibar na wimbo maalum.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Vijana ni nguzo ya rasilimali watu; tuwaamini, tuwawezeshe na tuwatumie kwa manufaa ya taifa letu.”.

 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...