Tuesday 10 December 2013

Video: R.Kelly amkumbuka Mandela kwa wimbo aliomuimbia walipokutana 2010 wakati wa kombe la dunia"

Ni vigumu kwa mtu yeyote kukataa kwamba Nelson Mandela ni Icon wa dunia, sio viongozi wakubwa, watu maarufu, matajiri, watu wa mataifa mbalimbali wameendelea kumkumbuka kwa njia mbalimbali kutokana na alivyomgusa kila mmoja. Mfalme wa R&B Robert Kelly hakuwa nyuma kutoa heshima zake kwa ‘tata’ Madiba.
kelly.R
Star wa ‘Coming To America’, Arsenio Hall (aliyeigiza kama Semmi) wiki iliyopita alidedicate talk show yake ya TV kwa Nelson Mandela.
Katika kipindi hicho, mfalme wa R&B R.Kelly alitoa heshima zake kwa Madiba kwa kuimba wimbo ‘Soldier’s Heart’ na kuzungumzia jinsi Rais huyo wa Afrika Kusini aliyepita alivyomu-inspire.
“I sang for Nelson Mandela in his home, out in Africa, during the time when I was doing the [2010] World Cup,” Alisema R.Kelly
R.Kelly alisema alikutana na Madiba wakati wa kombe la dunia 2010, fainali zilizofanyika nchini Afrika Kusini, na akiwa nyumbani kwake alimuimbia wimbo huo huku akipiga piano ya Madiba.
“And I sang a special song for him on his piano. I’m just blessed to know that I walked in his presence . . . and being around him inspired me to even go further in my life in my walk and my career and everything, man. He’s just an incredible power.” Alisema Kelly
Baada ya kumaliza kuimba, Hall alimuuliza Kelly kama anakumbuka Mandela alitoa reaction gani baada ya kumuimbia,
“He just nodded his head, man. He was very happy and very honored, as I was being in his presence. When I started performing the song on his piano, it was an unbelievable moment for me, man, as it is now.” Alisema R.Kelly

R.Kelly akimuimbia Mandela
R.Kelly akizungumza na Arsenio kuhusu Mandela
SOURCE: ROLLINGSTONE

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...