Thursday, 26 December 2013

WENGI WAJITOKEZA KUUGAGA MWILI WA ALIYEKUWA KOCHA WA MAKIPA SIMBA MAREHEMU JAMES KISAKA

 Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kocha wa makipa wa Simba, marehemu James Kisaka likiingizwa kwenye basi la klabu hiyo, baada ya kutolewa heshima za mwisho katika misa iliyofanyika katika Kanisa la Muhimbili, Dar es Salaam. Marehemu Kisaka atasafirishwa kwenda kwao wilayani Muheza, Tanga kwa mazishi yatakayofanyika kesho. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mjane wa marehemu James Kisaka, Teddy Kisaka akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mumewe

Mjane wa marehemu James Kisaka, Teddy Kisaka akifarijiana na mtoto wa pili wa marehemu Kisaka, Boniface baada ya kutoa heshima za mwisho.

 Ndugu wa karibu wa marehemu Kisaka akilia alipokuwa akitoa heshima za mwisho
 Mtoto wa mwisho wa marehemu Kisaka, Christopher akitoa heshima za mwisho
 Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited, Juma Pinto (kushoto), akisalimiana na Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba, Hassan Dalali.
 Wachezaji soka wa zamani wakijadiliana jambo nje ya Kanisa la Muhimbili walipokwenda kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James Kisaka. Kutoka kushoto ni Madaraka Selemani, Peter Tino, Khamis Kinye, Bakari Malima na Thomas Kipese.
 Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio', (kushoto) akijadiliana jambo na baadhi ya wachezaji wa soka waliokwenda kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James Kisaka.
 Benny Kisaka ambaye ni mdogo wa marehemu James Kisaka akisoma wasifu wa marehemu kakake
 Msanii wa filamu Jacob Steven JB akitoa heshima za mwisho
 Mchezaji wa zamani wa Simba Malota Soma akitoa heshima za mwisho kwa mchezaji mwenzie marehemu Kisaka.
 Mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la Jambo Leo, Asha Kigundula akitoa heshima za mwisho
Benny Kisaka ambaye ni mdogo wa marehemu, akitoa taarifa ya usafiri wa kwenda kwenye msiba baada ya kutoa heshima za mwisho. 


No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...