Sunday, 19 January 2014

BARABARA YA MASASI -TUNDURU!


Picha hii  kutoka kwa Maggid Mjengwa imenikumbusha safari yangu ya mtwara-Tunduru.Barabara hii huwa haipitiki wakati wa mvua.Usafiri kutoka Masasi-Tunduru ulikuwa wa land rover tu(110) na hakuna basi sijui kama kwasasa kuna mabadiliko kwani nipipita barabara hii 2004. Kuna mengi aliyonishangaza katika safari kati ya Tunduru-Masasi ila kubwa ilikuwa jinsi wanavyowasilisha barua kutoka sehemu moja kwenda nyingine!
Barua kwenda katika vijiji vilivyoko kati ya Tunduru na  Masasai zilifanywa kutupwa pembeni mwa barabara mara landrover inapofika katika kijiji husika.


 Niliuliza kwanini wanafanya vile na nikajibiwa kuwa ule ulikuwa ndio utaratibu wao wa kuwasilisha barua na barua itamfikia msomaji bila a wasiwasi.Ama kweli katika safari hii nilijifunza na kuona mengi na ninaweza kuandika kitabu kwani Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!Asante Maggid kwa ku-share picha na wasomaji.

Kopjes between Tunduru and Masasi
Barabara ya Masasi-Tunduru

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...