Wadau,swala la ajali limezidi kuwa tatizo kubwa nchini kwetu kwani kila kukicha ni lazima tutasikia kuna ajali ya gari imetokea mahali.Hivi nini ni chanzo cha ajali hizi zisizokwisha? Je,ni kweli kwamba tumeshindwa kabisa kutatua tatizo hili? Maisha ya watu yataangamia mpaka lini?Hivi tuna watu wangapi ambao wamepata ulemavu wa kudumu kutokana na ajali hizi? Je,ni watoto wangapi wamebaki yatima kutokana na ajali hizi?Binafsi nashindwa kuelewa kuwa tatizo ni kutokuwa na madereva wenye kiwango kinachotakiwa au magari mabovu,ama vyote kwa pamoja.
Kitu kilichonishangaza zaidi ni kuona kuwa gari hizi ndogo aina ya Toyota Noah kutumika kama gari za abiria!Ni nani ametoa kibali katika biashara hii?Alifikiria mbali au aliangalia nini?Kwa mtazamo wangu gari hii inatakiwa kutumika kwa matumizi ya kawaida ndani ya mji na si kufanya safari za masafa marefu na abiria.Kwa mara ya kwanza niliambiwa gari hizi zinabeba abiria kati ya Tanga na Korogwe nikashangaa na kutokuamini.Nilipoona taarifa ya ajali mbaya ya Singida ndipo nikakumbuka.Watu wasiokuwa na hatia wamepoteza maisha kwa tatizo ambalo lineweza kuzuiwa.Mungu azilaze roho za marehemu wote wa ajali ya Singida mahali pema peponi,amen.
Wadau,tujadili nini kifanyike ili kupunguza tatizo hili.Unaweza kutuma maoni yako na tutayatoa hapa.Nakaribisha mjadala ili tunusuru maisha yetu!
Noah ilivyo nje
Noah ilivyo ndani
Kupakia abiria humu si kutafuta majanga wadau?Hii ni gari ya familia na si abiria wa masafa marefu.
No comments:
Post a Comment