Komla Dumor |
Komla na Morgan Tsvangirai katika studio za BBC London
Mwandishi wa BBC Komla Dumor amefariki ghafla nyumbani kwake kutokana na mshtuko wa moyo.
Alikuwa na miaka 41 alipopata mauti yake.Komla Dumor ameelezewa kuwa miongoni mwa waandishi shupavu barani Afrika.
Rais wa Ghana John Dramani Mahama amemtaja marehemu kama zawadi ya Ghana ulimwenguni na kuongezea kuwa Ghana imempoteza mmoja wa wajumbe wake.
Komla hivi karibuni alikuwa anaongoza kipindi cha Runinga kinachozungumzia maswala ya Afrika baada ya kufanya kazi katika radio mmoja nchini Ghana na vilevile radio ya BBC.
Mhariri wa habari za ulimwengu Andrew Whitehead amemtaja kuwa mwadishi shupavu aliyekuwa na uhusiano mzuri na wasikilizaji.
CHANZO: BBC
No comments:
Post a Comment