Saturday 4 January 2014

Mwili wa Dkt. William Mgimwa Wawasili Kutoka Nchini Afrika Kusini



Ndege iliyoubeba mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. William Mgimwa Ilipowasili katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Leo Kutokea Nchini Afrika Kusini alipokutwa na Mauti siku chache zilizopita.
Mjane Mama Jane Mgimwa(katikati) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Afrika kusini Radhia Msuya(kulia) mara baada ya kuwasili kutoka nchini Afrika kusini
Naibu Waziri Wizara ya Fedha Saada Mkuya(kulia) akimsindikiza Mke wa Marehemu Mama Jane Mgimwa(katikati)katika chumba cha mapumziko mara baada ya kuwasili katika katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Leo.Kushoto ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mh. Sophia Simba.


Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wabunge waliojitokeza kuupokea mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa.
Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue akitoa heshima kwa kugusa Jeneza Lililobeba mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu  Dkt. William Mgimwa Katikati ni Waziri wa Ujenzi Mh. John Magufuli na wa Mwisho ni Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mh.Fenella Mukangara.
Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. William Mgimwa Ukiingizwa kwenye gari Maalum Tayari kwa ajili ya kuelekea nyumbani kwa marehemu kwa taratibu nyingine za mazishi.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (wa kwanza Kushoto)akisalimiana na baadhi wa Watu waliofika kuupokea Mwili wa wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. William Mgimwa Leo Jijini Dar es Salaam.

                                                            Picha na Hassan Silayo-MAELEZO

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...