Wednesday, 22 January 2014

Tanzia: Saidi Ramadhani Bwanamdogo, Mbunge wa Chalinze

Picture: Saidi Ramadhani Bwanamdogo
Saidi Ramadhani Bwanamdogo (24.12.1968 - 22.01.2014)
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne S. Makinda (Mb), anasikitika kutoa taarifa ya kifo cha Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Saidi Ramadhani Bwanamdogo Kilichotokea leo (Jumatano) asubuhi tarehe 22.1.2014 Katika hospitali ya Muhimbili/MOI alikokuwa amelazwa kwa Matibabu.

Mipango ya Mazishi zinaendela kufanywa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya Marehemu, ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho siku ya Alhamisi tarehe 23 Januari, 2014 kijijini kwake MIONO, Wilaya ya BAGAMOYO, Mkoa wa PWANI. Taarifa zaidi juu ya msiba huu zitaendelea kutolewa na Ofisis ya Bunge kadrizitakapopatikana.

Inna llilah Waina Illaih Rajiun!”

Imetolewa na

Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusianao wa Kimataifa,
Ofisi ya Bunge,
DAR ES SALAAM
22.01.2014

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...