Rais Jakaya Kikwete ametoa ujumbe mzuri na wa maana mno kwa wajumbe wa baraza la vyama vya siasa.Kwangu mimi ujumbe huu ni wa maana kwa wale wote watakaoshiriki katika bunge la katiba kutuwakilisha.Wawakilishi wetu ni lazima wajue kuwa wanakwenda kutengeneza katiba kwa maslahi ya watanzania na si vinginevyo.Kama mtu anadhani kuwemo katika bunge la katiba ni kukipaisha chama chake au taasisi anayotokea ni bora akatae uteuzi pale atakapoteuliwa na rais.Hatungependa kuona malumbano yasiyokuwa na maana kama wanavyofanya baadhi ya wabunge kwenye bunge la bajeti.Kama mtu anaona kwenda bungeni na kuongea ilimradi aonekane katika runinga basi ajiunge na vikundi vya sanaa vinavyoonyesha michezo ya kuigiza katika runinga na tutamwona,asikanyage kabisa katika bunge la katiba maana si mahali pake.
Bunge la katiba linahitaji watu wenye uzalendo wa kweli na wanaoitakia mema nchi yetu na watu wake.
Hotuba hii ni muhimu kuangaliwa na kila mmoja wetu.
Mungu ibariki Tanzania.
No comments:
Post a Comment