Friday, 7 February 2014

THE LIVING ROOM: JINSI YA KUCHAGUA MAPAZIA

Kama kuna kitu ninachokipenda ndani ya nyumba basi ni mapazia.Hii inanipelekea kununua mapazia ya aina tofauti mara kwa mara,Katika upangiliaji wa mapazia yangu nyumbani kwangu huwa ninazingatia rangi katika kuta, mazulia, na samani(fenicha).Nadhani kila mtu ana mtazamo wake ila kwa kweli ili upate mpangilio ulio mzuri inabidi usigonganishe sana rangi kwani unaweza kufanya nyumba yako iwe na giza sana au ionekane kama chafu. Wengi wetu huwa tunashindwa kujua tuweke mapazia ya aina gani.Huwa inakuwa ngumu sana kwa wale wenye samani hususan masofa yaliyotengenezwa kwa vitambaa vya maua.Naweka baadhi ya picha hapa kukusaidia kidogo msomaji wangu katika kupangilia  na nitakuwa nafanya hivi mara kwa mara.


















No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...