Friday 4 April 2014

WAATHIRIKA WA MILIPUKO YA OSAMA DAR WAFURAHIA FIDIA



Mjane wa Abasi Mwila, Judith Mwila akipanga bidhaa katika genge lake lililopo Tabata Liwiti jijini Dar es Salaam jana. Judith ni miongoni mwa watu tisa watakaonufaika na fidia ya Sh672 bilioni baada ya kumpoteza mume wake, Abasi katika shambulio la kigaidi la mwaka 1998 kwenye ubalozi wa Marekani nchini. Picha na Michael Jamson 


Dar es Salaam. Baadhi ya wanafamilia wa waliopoteza ndugu kwenye shambulio la ugaidi katika Ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam mwaka 1998, wameelezea kufarijika kutokana na malipo ya fidia, licha ya kwamba hayawezi kurejesha uhai wa waliokufa.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, ndugu hao walisema, licha ya mahakama nchini Marekani kuwapa fidia lakini pengo la jamaa zao halitazibika.
Wiki iliyopita, Mahakama Kuu ya Marekani, ilitoa amri ya kuwalipa fidia ya dola za Marekani 957 milioni (Sh1.555 trilioni) waathirika 23 wa shambulio hilo.
Kwa habari zaidi ingia: www.mwananchi.co.tz

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...