Hali
ya msichana Yusta Lucas mwenye umri wa miaka 20
aliyefanyiwa ukatili wa
kufungiwa ndani kwa zaidi ya mwaka mmoja
huku akipewa adhabu ya kunga'twa na kuchomwa kwa pasi na mwajiri wake Amina Maige wa Mwananyamala jijini
Dar es salaam inaendelea vizuri kufuatia
matibabu anayopata ya majeraha yaliyomsababisha kupoteza fahamu.
ITV
imefika katika hospitali ya Mwananyamala alikolazwa binti huyo mzaliwa wa
Tabora na kuweza kufanya nae mahojiana ambapo akiongea kwa tabu amesema alianza
kuishi na mwajiri wake tangu mwaka 2011 bila kuruhusiwa kutoka nje ya njumba
waliyokuwa wanaishi ama kuwasiliana na ndugu zake na hata kurudi kwao ambpo
mwajiri wake huyo alifiki kipindi akabadilisha adhabu pindi anapofanya makosa
na kumwadhibi kwa kumuuwa kwa meno yake na kumchoma kwa pasi na maji ya moto.
Mganga
mfawidhi hospitali ya mkoa Mwananyamala amesema hali ya binti huyo inaendelea
kuimarika baada ya kuanza kupewa matibabu na kubaini tayari alikuwa
ameshaadhirika kisaikolojia kiasi cha kuogopa hata kuangalia watu kutokana na
kutoanana na watu kwa muda mrefu.
Mkaguzi
msaidizi wa polisi dawati la jinsia Prisca Komba amesema walifanikiwa kujua
mateso ya binti huyo baada ya kupewa taarifa na msamaria mwema ambaye alikuwa
jirani yake na kuwa uchunguzi bado unaendelea wakati mtuhumiwa akiwa bado
rumande na kutoa wito kwa jamii kuendelea kuibua matukio kama hayo ili
watuhumiwa waweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Afisa
programu kituo cha sheria na haki za binadamu bi Naemy Sillayo amaesema wao
kama kituo cha kutetea haki za binadamu wameendelea kusikitishwa na vitendo
vinavyotokea hapa nchini na kutoa wito kwa jamii kuviibua.
CHANZO: ITV
No comments:
Post a Comment