Chai ya hibiscus Maua ya hibiscus yaliyokaushwa
Ua la hibiscus
Hibiscus ni ua ambalo lilikuwa halikosekani nyumbani kwetu.Tulikuwa na hibiscus za rangi mbalimbali.Baba yangu alikuwa ni mpenzi sana wa maua hivyo nyumbani kwetu tulikuwa na bustani kubwa yenye maua aina tofauti kuanzia bouganivillea, jasmine, money plant zenye majani makubwa na madogo, maua ridi(roses) za rangi mbalimbali na mengine mengi ambayo kwa kweli sikujua majina yake.Vilevile tulikuwa na miti mbalimbali ikiwemo ya matunda kama malimao,machungwa,ndimu, mastafeli nk.
Mapapai tulikuwa hatununui sokoni kwani tulikuwa na miti ya mipapai ya kila aina.Vilevile tulikuwa na migomba ya kutosha hali iliyopelekea kutokununua sana ndizi mbivu.Ndizi za kupika ndiyo tulikuwa hatununui kabisa hii ni kutokana na kuwa wanafamilia wengi tulikuwa hatupendi nzdizi za kupikwa husan ndizi mbichi!Ila kwasasa mimi ni mpenzi sana wa ndizi mbichi ILA baadhi.
Tulikuwa na aina tofauti za ndizi kama ndizi Bukoba(ambazo mama yangu alizipenda sana), mkono wa tembo, kisukari,malindi n.k
Tulikuwa na mihogo mingi ya kutuwezesha kupata kisamvu cha kukidhi matumizi ya familia.Tulikuwa na matembele pamoja na mboga ya maboga.
No comments:
Post a Comment