Friday 13 February 2015

MADA YA SIKU: JE, KUNA UMUHIMU WA KUWA NA PF3?

Nimekuwa nikitatizika sana na swala la PF3,nadhani wengi tunajua kuwa ni kitu gani. Hivi ni haki kukimbilia polisi kuchukua PF3 kwanza badala ya kumkimbiza majeruhi hospitali?Hii imekaaje wadau.

Majeruhi wengi ambao wamepoteza maisha wangeweza kuokolewa kwa wakati kama si kukimbilia PF3 kwanza katika vituo vya polisi badala ya kukimbilia hospitali kwanza. Hata waliopewa sumu n.k wanaweza kuokolewa katika muda mwafaka.

Siwezi kusema moja kwa moja kama wazo la kuwa na PF3 halifai sababu sijui walioweka walikuwa na makusudi gani bali ninaweza kutoa mawazo yangu katika hili.Nadhani ingekuwa vyema polisi wakaweka dawati lao katika hospitali zote muhimu na kutoa hizo PF3 sambamba na majeruhi kuhudumiwa ili kuokoa maisha ya majeruhi.

Kwa mfano majeruhi anayetokwa na damu kwa wingi anaweza kusaidiwa kuzuia utokaji wa damu hiyo na hapohapo kupewa damu nyingine na hivyo kuokoa maisha yake.Huwezi kuokoa maisha ya majeruhi huyu kwa kukimbilia kituo cha polisi kwanza kuchukua PF3!.



Je, wewe mdau una mawazo gani?

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...