Wednesday 11 February 2015

MADA YA SIKU: NI HALALI MTU KUGONGWA KATIKA ALAMA YA PUNDAMILIA?

Pundamilia ni moja katika alama za barabarani.Alama hii ina maana ni sehemu ya kuvuka waenda kwa miguu na magari hutakiwa kusimama.Nimekuwa nikishangazwa mara kwa mara kusoma kuhusu watu kugongwa na magari katika alama hizi.Nimeshuhudia mwenyewe vilevile jinsi madereva wanavyokaidi kusimama katika alama hizi.Madereva wanapita kama vile hakuna alama yeyote.Hii inasikitisha sana.Maana inaleta maana kuwa barabara ni haki ya waendesha vyombo vya moto na si kwa watembea miguu. Sweden,alama za barabarani zinaheshimika mno.Madereva wanazingatia sana mwendokasi ulioweka mfano katika eneo la shule ambapo magari hutakiwa kutembea  si zaidi ya  kilomita 30 kwa saa. Kwenye alama ya pundamilia,hata kama wewe mvuka kwa miguu utaona gari inakuja  na kuwa na shaka kuwa dereva atapita,huwa haiwi hivyo.Dereva atasimama na kukuonyesha ishara ya kuvuka! Sweden, kosa la dereva kuzembea katika alama za barabarani hupelekea dereva huyo kufungwa jela na kupoteza leseni. Na hata ukitaka kupata leseni tena baada ya kutumikia adhabu inabidi ufuate taratibu upya kama mtu asiyekuwa na leseni.Taratibu zenyewe zina mlolongo mrefu na ni gharama.

Inasikitisha nchini kwetu kuona watoto wa shule wanagongwa na kufa tena nje ya shule zao.Hivi hawa wanaogonga watoto na raia wengine katika alama za pundamilia huchukuliwa hatua gani?Au ndiyo marehemu hana haki?

Nadhani imefikia wakati wa kubadilishwa kwa sheria za barabarani zisizokidhi nchini Tanzania.Nina imani sheria  ngumu zitapunguza sana ajali za barabarani.


Je,sheria zetu zikoje?

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...