Safari moja nilikuwa
nasafiri kikazi kutoka wilaya ya Tunduru kuelekea mtwara. Barabara ya
Tunduru-Masasi ni moja ya barabara zilizokuwa mbaya sana.Sijui kwasasa iko vipi
maana hiyo ilikuwa ni miaka 10 iliyopita. Tulikuwa katika landrover 110. Tulipita
vijiji mbalimbali. Baada ya kwenda kwa muda,dereva wa gari yetu alisimama katika
kijiji kimoja na kutupa barua pembeni mwa barabara.
Barua hizo alizitia katika
mfuko wa plastiki unaaonyesha. Mimi nilishangaa na kumuuliza dereva,alikuwa
amefanyanini? Akaniambia,”dada,huku barua nyingi za wakazi wa vijiji hivi
zinaletwa kwa namna hii na hakuna barua inayopotea labda itokee bahati mbaya.
Mkazi yeyote wa kijiji akipita, anaokota barua na kuzifikisha kwa
mhusika/wahusika. Na
nimeziweka katika mfuko wa plastiki ili hata kama mvua itanyesha barua ziwe
salama”. Kwa kweli nilishangaa sana ila nilifurahishwa kwa wakazi kuwa na
utaratibu wao mzuri wa kuhakikisha kuwa umbali,ubovu wa miundo mbinu haukuwa
kikwazo kwa wao kupata mawasiliano kutoka kwa jamaa zao n.k
KWELI TEMBEA UONE!
No comments:
Post a Comment