Tunduru mjini
Nilipokuwa katika
wilaya ya Tunduru kikazi nilikutana na salam ambayo ilinitatiza.Kweli tembea
uone.
Ilikuwa ni asubuhi ya siku ya pili toka nifike wilayani Tunduru. Mmoja wa
wafanyakazi wa hoteli niliyofikia alinisalimia, ”dada habari za mwili?”
Kwa kweli nilitoa macho kwanza na sikujua nimjibu nini. Nilijiuliza alikuwa
na maana gani kuniulizia habari za mwili? Nikiwa ndani ya mshangao nilimjibu
nzuri ila sikuwa na uhakika na jibu langu.
Baada ya jibu hilo akaniuliza tena, ”za muamko?” Hahaha
Nikasema leo nimepatikana. Nikamjibu, ”nzuri”. Ila kama jibu la kwanza,
sikuwa na uhakika na jibu langu.
Nilipoenda kukutana na wafanyakazi wenzangu,niliwaelezea yaliyonikuta.
Walicheka sana na kuniambia kuwa hiyo ilikuwa ni salam ya kawaida kabisa ya
wakazi wa Tunduru.Na kuwa nilijibu sawa.
KWELI TEMBEA UONE.
Imeandikwa na Anna
Nindi
No comments:
Post a Comment