Wednesday 25 March 2015

FAIDA ZA MAFUTA YA UBUYU/UNGA WA UBUYU

Yana Virutubisho Vifuatavyo:
  • -Vitamin:  (Thiamin) vitamin B1, Riboflavin) B2, (Niacin) B3, kiasi kikubwa cha (Ascorbic Acid) Vitamin C, Vitamin A, Vitamin D, Antioxidant na Vitamin E (Tocopherol)
  • -Madini kama vile: – kiasi kikubwa cha Calcium, Manganese, Iron, Potassium, Zinc, Phosphorus, na Amino acids 

FAIDA ZAKE:- 
  • Yanakuongezea hamu ya kula na kukumbuka vizuri kwa ufasaha kutokana na kiwango kikubwa cha vitamin B complex zilizomo. kwa hiyo ni mazuri kwa wakubwa na watoto
  • Yanasaidia kunyonywa kwa vitamin B12 kwenye tumbo kutokana na kiwango kikubwa cha ascorbic acid, ambayo ni muhimu kwenye kutengeneza chembe hai nyekundu na kukuepusha na Anemia.
  • Yanasaidia kusafisha mfumo wa chakula na kufunga tumbo la kuhara zaidi kwenye unga  wa ubuyu kutokana na uwepo wa “roughage” nyingi.
  • Yanasaidia mtu  kuona vizuri kutokana na uwepo wa Vitamin A ndani yake.
  • Mazuri kwa Walemavu wa Ngozi kama (Albino) Kutokana na uwepo wa vitamin A, Vitamin D na Vitamin E (Tocopherol).
  • Ni mazuri pia kwa watoto wadogo na  wajawazito kwa ajili  ya kuimarisha mifupa hasa  kuanzia miezi sita hadi tisa ya ujauzito (third tremester), hiki ni kipindi ambacho mtoto anatengeneza na kuimarisha mifupa yake akiwa tumboni kwa mama yake, hii ni kwasababu ya kiwango kikubwa cha Calcium na vitamin D, na vitamin A.
  • Mafuta haya ni mazuri kwa kupunguza vitambi kutokana na uwepo wa Omega 3.
  • Hurekebisha kiwango cha sukari mwilini.
  • Hurekebisha shinikizo la damu (pressure).
  • Yanasaidia kuongeza kinga ya mwili yaani CD+4, zaidi kwa wagonjwa wa ukimwi, kansa, au watu waliougua kwa muda mrefu na wanawake wanapokuwa katika hedhi wanaweza kutumia.

MATUMIZI:-Tumia vijiko viwili vya mafuta kwenye kijiko cha chai, kisha changanya kwenye glasi ya maji, juisi, maziwa,( yanaweza kuwa mtindi au freshi), soda, asali n.k, au unaweza kunywa bila kuchanganya na kitu kingine. Tumia hivyo  mara mbili kwa siku asubuhi na jioni kwa mafanikio mema na matokeo mazuri.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...