Ninaendelea kushirikiana na nyie mapishi yangu mwenyewe
jikoni kwangu. Nitakuwa ninafanya hivi kila nitakapopata
nafasi.
MAHITAJI
1 Samaki (
Sato,changu n.k)
½ kg viazi
mviringo
1 pilipili hoho ya
kijani
1 karoti kubwa
1 kitunguu maji
cha ukubwa wa kati
2 nyanya ukubwa wa kati
½ kikombe njegere(ukipenda)
1 kjc chumvi(unaweza kuongeza/kupunguza kulingana na matakwa yako).
1 pilipili mbuzi mbichi(ukipenda)
1 lita maji(unaweza kuongeza kama mchemsho utakuwa haujaiva)
1 kidonge cha supu(stock) ya samaki(kupata ladha nzuri)
FANYA HIVI
Menya viazi na vikate katika vipande.
Osha samaki wako vizuri. Muweke pembeni.
Osha nyanya, hoho na katakata kila kimoja katika vipande vidogo wastani.Weka
pembeni.
Katakata kitunguu katika vipande vidogo.
Weka vitu vyote katika sufuria isipokuwa chumvi, kidonge cha supu ya samaki
na pilipili mbuzi. Ongeza maji.
Funika na acha vichemke kwa dakika 30.Weka kidonge cha supu ya samaki,
chumvi na pilipili mbuzi.Maji yaliyomo katika mchemsho kama hayatoshi unaweza
kuongeza mengine ili upate supu ya kutosha.
vidonge(blocks) vya samaki au fish stock
Mchemsho wako ni tayari! Pata na glasi ya juisi ya matunda fresh.
Ni chakula kizuri sana kiafya kwa maana hakuna mafuta ya kutengenezwa na
kuna mboga nying ina samaki ambazo vyote ni virutubisho tosha.
DOKEZO: Badala ya
viazi unaweza kutumia ndizi mbichi(green banana) vilevile. Na badala ya samaki
unaweza kutumia nyama ya kuku, nyama ya ng´ombe n.k
Mpishi: Anna Nindi
No comments:
Post a Comment