Thursday, 26 March 2015

JUISI YA NANASI NA UKWAJU

MAHITAJI
100g Ukwaju 

200g Sukari

1 nanasi dogo( ½ kubwa)


Flavour unayopenda( vanila etc)

Namna ya kutayarisha na kutengeneza

Roweka ukwaju na sukari kwa maji ya moto na uwache kwa nusu saa.

Menya nanasi na ulisage kwenye blender ili upate juice. Ichuje juisi
 yako.Weka pembeni juice ya nanasi.

Saga ukwaju uliorowekwa na sukari  kwenye blender. 

Ichuje juice hiyo ya ukwaju.Weka pembeni.

Changanya juice hizo mbili na umalizie kwa kuweka flavour uipendayo. 

Koroga vizuri na weka barafu na tayari kwa kunywewa.
Unaweza kunywa juisi hii na vitafunwa mbalimbali kama sambusa, kababu n.k

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...