MAHITAJI
Dagaa 1/4 kg
Pilipili hoho 1 kubwa
Nyanya 3
Kitunguu 1 kikubwa
Karoti 1kubwa
Mafuta ya kipikia 1 dl
Chumvi kissing upendacho
Limao/ndimu kipande
Tandoori Masala kijiko 1 change chakula
Tangawizi/kitunguu swaumu (sio lazima)
FANYA HIVI
Osha dagaa kwa maji ya vuguvugu mpaka uhakikishe Hawana michanga.
Katakata Nyanya, vitunguu, hoho na karoti ktk mtindo unaotaka.
Weka sufuria jikoni na Mafuta ya kipikia.
Weka vitunguu na kaanga mpaka viwe kahawia.
Ongeza Nyanya na kaanga mpaka ziive.Weka Chumvi kupata ladha
Weka Dagaa wako na Tandoori Masala na juisi ya ndimu/limao
Kaanga kidogo halafu weka maji katika mchanganyiko wako. Acha uchemke mpaka maji yaanze kukauka.
Angalia kama Dagaa wameiva.Kama bado,Ongeza maji.
Kama wameiva,weka Karoti na Pilipili hoho na aacha mchanganyiko uchemke kwa dakika 5.
Dagaa wake ni tamarind kwa kuliwa.
Mimi hupendelea kula na ugali na mboga ye yote ya majani.
No comments:
Post a Comment