Wanandoa waliotalikiana
Watu walio katika talaka wana uwezekano mkubwa wa kupatwa na ugonjwa wa mshtuko wa moyo ukilinganisha na wenzao ambao bado wako katika ndoa ,kulingana na utafiti nchini Marekani.
Utafiti uliofanyiwa watu 15,827 unaonyesha kuwa wanawake ndio walioathirika zaidi na kwamba hupunguza hatari hiyo baada ya kuolewa tena.
Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Journal unasema kuwa msongo wa mawazo kupitia kiasi unaohusishwa na talaka una athari za mda mrefu katika mwili.
Wakfu wa moyo nchini Uingereza umetaka kufanyika kwa utafiti zaidi kabla ya talaka kuorodheshwa miongoni mwa tishio la mshtuko wa moyo
Wakati wa utafiti huo uliofanyika kati ya mwaka 1992 na 2010,mmoja kati ya watu watatu hutalakiana .
Asilimia 24 ya wanawake wanaotalaki mara moja hukabiliwa na tishio la ugonjwa huo wa moyo ikilinganishwa na wanawake ambao wameolewa.
Takwimu hizo pia zinasema kuwa wale ambao wamekuwa na misururu ya talaka wako asilimia 77 kupatwa na ugonjwa huo.
chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment