Wednesday, 8 April 2015

TEMBEA UONE: UGEMAJI WA POMBE YA MNAZI

Mgemaji akionekaja juu ya mnazi

Kutembea kunafundisha vitu vingi sana.Na hiki ndicho nilikuwa ninafurahia katika safari zangu zote.Kwa kweli kwa Tanzania nilibahatika kutembea sana hivyo kuona jinsi maisha yalivyo katika maeneo tofauti. Nikiwa Turiani Morogoro jioni moja baada ya shughuli za kazi iliyonipeleka kule tulikaa mahali kupata nyama choma/ chakula. Tulikuwa tumekaa nje kwenye meza yetu tukisubiri chakula chetu. 


Turiani kuna minazi mingi na hata jirani na eneo tulilokuwa tumekaa palikuwa na minazi vilevile. Tukiwa tumekaa tukaona mtu anapanda mnazi huku kiunoni kukiwa kuna ning´inia kisu  pamoja na  chombo cha  plastiki. Chombo cha  plastiki kilitokana na kopo la mafuta ya kula mfano KORIE, SUNFLOWER, ROKI n.k.

Yule mtu alipofika juu ya mnazi, hatukuelewa alikuwa anafanya nini ila baada ya muda tukaona anashuka akiwa hana lile kopo. Baada ya muda tukamwona anapanda mnazi mwingine na kufanya yale aliyofanya katika mnazi wa awali. Nilipomwona Yule mtu nikakumbuka kitu,kuwa katika siku zilizopita niliona watu wengine wakipanda minazi na makopo na kushuka bila ya makopo. Halafu nikawaona wengine wakishuka na makopo. Palepale nikapata swali la kumuuliza mwenyeji wetu ambaye tulikuwa nae pale kuwa nini wale watu walikuwa wakipeleka na makopo yao juu ya mnazi?
Jibu kutoka kwa mwenyeji wetu likawa watu wale walikuwa “wakigema” pombe ya mnazi!Walikuwa wanakinga pombe hiyo kwa kuweka chombo kile na plastiki kwa muda waliojua wao  na baadae walirudi kuchukua kilichopatikana. Nilikuwa najua kuna pombe ya mnazi ila sikujua upatikanaji wake.
Ila ni njia ya hatari kwa kweli maana mgema anaweza kuanguka na kupoteza maisha.

KWELI TEMBEA UONE!

Imeandikwa na Anna Nindi

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...