Nilitembelea Makambako,iliyopo
mkoani Iringa.Nilikuwa na safari ya Makambako, Songea na Mbeya. Makambako pana
baridi nyakati za jioni hasa katika kipindi nilichokwenda,mwezi wa agusti kama
sikosei.Jua lilikuwa kali sana mchana.
Nikiwa Makambako nikapewa stori
ya kutisha kidogo kuwa wamiliki wengi wa maduka pale Makambako,walikuwa
wanatumia ushirikina kufanya biashara zao. Mojawapo ya ushirikina waliokuwa
wanafanya ni mnunuzi unapokwenda dukani,basi mwenye duka atakuona ukiwa
mtupu(ukiwa huna nguo).Je,walifanya hivi kwaajili ya nini? Jibu ni kuwa,kwa
kufanya hivi walivutia wateja zaidi na kuuza zaidi.Niliogopa kwa kweli ila
sikujua kama ni kitu cha kweli au la.
Nilijiuliza maswali mengi kuwa
kwanini mtu afanye biashara kishetani namna hii? Je,wateja waliojua hili(kama
ni kweli),walijisikiaje walipokuwa wakienda madukani? Jamani,ni stori
niliyopewa na wenyeji,hivyo sina uthibitisho.
KWELI TEMBEA UONE
Imeandikwa na Anna Nindi
No comments:
Post a Comment