Nadhani ni wakati mwafaka wa kuwa
na taasisi/vyombo vingi visivyo vya kiserikali ili kushughulikia maswala ya
sheria za mirathi kwa wanawake wajane. Inasikitisha kuona mwanamke amechuma mali
na mumewe kwa taabu ndugu za mume wakiwa na yao halafu anapofariki mume wao
wanajileta kurithi mali.Mali ipi hapa? Jamani watu hawana aibu hivi. Marehemu
kaacha mke na watoto wake na hao ndiyo warithi halali wa mali. Sasa hawa ndugu
za mume wakichukua mali ambayo wala hawakuichuma,watoto wataishi vipi? Watu
waache kubweteka na kusubiri mali za kurithi.
Nimeupenda ujasiri wa mwanamke wa
mwisho katika video hiyo hapo juu.Yeye aliamua kukomaa na wapenda vya
bure.Tuwasaidie wale wasioelewa haki zao.
Mwanaume jasiri hutafuta mali
yake mwenyewe kwa jasho lake na mtegemea cha ndugu siku zote,hufa masikini.
Badilikeni!
No comments:
Post a Comment