Miswak
Mswaki (inatokana
na neon la Kiarabu miswaq), ni kijiti kibichi ambacho kinatokana na mti au kichaka na
kisha kutafunwa upande mmoja na hutumika
kusafishia meno kutokana na mabaki ya chakula yanayoweza kuyaharibu.
FAIDA ZA
MSWAKI
Inasemekana mswaki unaimarisha ufizi (nyama inayoshikili
meno), unazuia uozo wa meno, unaondoa maumivu ya meno na harufu mbaya kinywani.
Hasa ukitokana na mti mswaki (Salvadora persica) (arak kwa Kiarabu) au miti mingine
maalumu kulingana na mazingira, kwa mfano msega au mkupa (Dobera glabra na D. loranthifolia), una sifa za muda mrefu
zinazoufanya uendelee kuwa mbadala wa miswaki ya kisasa, ikiwepo ile inayotumia
umeme.
Unatumika hasa Uarabuni, Afrika Kaskazini, kwenye Sahel na
Pembe ya Afrika, India, Asia ya Kati, Asia ya Kusini Mashariki.
KAULI YA WANASAYANSI
World Health Organization (kifupi WHO, yaani Idara ya Afya ya
Umoja wa Mataifa) ilihamasisha matumizi ya mswaki mwaka 1986.
Mwaka 2000 ripoti ya kimataifa kuhusu usafi wa kinywa
ilionyesha makubaliano ya kwamba unahitajika utafiti zaidi kuthibitisha faida
ya mswaki.
Utafiti wa mwaka 2003 ulionyesha kwamba matumizi sahihi ya
mswaki asili yalikuwa na manufaa kuliko miswaki ya kisasa. Hata hivyo, utafiti
uliishia kupima watu 15 tu, idadi isiyotosha kabisa kama uthibitisho.
Matumizi
Ingawa wengi wanapiga mswaki hasa asubuhi wanapooga au kunawa,
halafu pengine huenda wakanywa chai ambayo inaacha sukari katika meno na hivyo
kuandaa uozaji wake, utaratibu sahihi ni kupiga mswaki baada ya chakula, hasa
cha jioni, kusudi meno yabaki safi muda wote wa usiku.
Kwa kulinda usafi, ncha ya mswaki inatakiwa kukatwa kila
unapotumika.
Usitunzwe kamwe karibu na choo au sinki.
Mswaki ukikauka unatakiwa kulainishwa kwa maji ya waridi.
CHANZO: Wikipedia
|
No comments:
Post a Comment