Hii supu ni
rahisi sana kutengeneza na ina virutubisho vyote.Ni mlo wangu sa mchana wa
leo.Ninakuandikia hapa upishi wake.
MAHITAJI( kwa watu 2)
½-1 kikombe Nyama ya kusaga
Pilipilimanga (weka kiasi
upendacho)
Chumvi (weka kiasi upendacho)
Mbogamboga nilizotumia
1 kitunguu maji
1 kitunguu maji
1 Karoti(ukubwa wa wastani)
¼ kikombe njegere
¼ kikombe French beans
1 kiazi chenye ukubwa wa kati
FANYA HIVI
- Katakata karoti, kiazi na kitunguu katika vipande vidogo vidogo
- · Weka nyama ya kusaga katika sufuria.Weka jikoni na acha nyama ichemke.
- · Tumbukiza mbogamboga zote ziendelee kuchemka na nyama.
- · Pika mpaka uone viazi vimelainika.
- · Weka chumvi na pilipilimanga kupata ladha
Supu yako
ipo tayari na unaweza kula yenyewe tu na ukashiba au ukala na chapati au mkate.
ANGALIZO:
Mbogamboga unaweza kutumia unazopenda kama: kabichi, brokoli, hoho n.k
Mpishi: Anna
No comments:
Post a Comment