Kuna
familia za ajabu kweli humu duniani. Utakuta mmezaliwa watoto kadhaa katika
familia yenu na wote mmekuwa na maisha yenu na mna familia zenu. Sasa kuna
ambao mbali na kuwa na familia zao, hutaka kuwatumia wenzao kama vitega
uchumi.Wao hujali maisha yao na ya watoto wao tu na hufanya lolote ili matakwa
yao yafanikiwe. Mfano ,kama wanakuona una unafuu wa maisha (wakati mwingine
siyo hivyo, wanakuona hivyo kutokana na msaada ulionao aidha kutoka kwa
mke/mume) basi watajaribu kukuhadaa katika kila kitu hususan wakijua una shauku
ya kujenga, kununua kiwanja n.k.Kinachotokea hapa hutapata kiwanja wala
nini.Pesa zako zitatumika zote maana familia yote imetolea macho pesa hizohizo
au wote wamejikusanya katika biashara ndogo ya familia ambayo kwa mtu mwenye
akili timamu ukiangalia unaona kabisa hakuna kinachoendelea hapo zaidi ya watu
kwenda kupunga upepo na kurudi nyumbani.Ndiyo hapo watakapokuua kwa shinikizo
la damu pale utakapodai pesa zako!Kwani utapigwa stori zisizoeleweka au
watafanya kila wawezalo kuhakikisha huendi katika eneo la tukio. Tujifunze kuwa
si ndugu wote wana nia nzuri kwetu,Kikubwa angalia familia uliyonayo yaani
mke/mume na watoto kwanza, na hapa ndiyo utapata maendeleo.Jaribu kutumia akili
yako mwenyewe na si kuburuzwa.Shirikiana kimawazo na mke/mume wako zaidi ili
kufikia malengo vinginevyo unastaafu ukiwa huna hata kibanda wala kiwanja ila
una mipango yako hewa isiyokamilika! Anaesikia na asikie.
Tuache kutumiana,tutafute kwa
jasho letu.
Asante mdau uliyetuletea kero hii.
No comments:
Post a Comment