Tuesday, 8 September 2015

KERO: WEMA HUNA NA HISANI HUKUMBUKI?

Kama kuna mtu mwenye kusahau haraka basi ni mwanadamu.Mtu unaanza maisha nae, hana mbele wala nyuma.Mnaishi kwa taabu na shida kwa kuvumiliana na kusaidiana.Unajitolea kwa hali na mali ili kuficha aibu ya mwenzako. Baada ya muda Mungu anawajalia maisha ya kuridhisha.Hapa ndiyo shughuli inapoanza.Uliyemsaidia mpaka kufikia hiyo nafuu ya maisha anasahau kila kitu.Wanaume wengi ndiyo wenye mambo haya.Unaanza kutafuta michepuko si unang´aa sasa na pesa za kubadilisha mboga unazo.Basi kama umenunua kijigari ndiyo kabisa.Unaona wewe maisha ndiyo umeyashinda.Hapo una kijigari lakini huna hata kiwanja !Sijui utaishi ndani ya hiyo gari?Badala ya kuwa na akili kuwa ukanunue hata kiwanja wewe unakwenda kutafuta wanawake. Halafu mtu anayefanya hivi ni mtu ambaye umri umekwenda,wala si kijana mdogo. Ameona UZINZI ndiyo maisha hajui kwamba kuna maisha zaidi ya huo UZINZI!

Ama kweli akili ni nywele na kila mtu ana zake.
Kibaya unamfukuza aliyekunyanyua mpaka ukafika hapo ulipo ETI uje uishi na mwanamke ambaye hajachangia lolote katika maisha yako zaidi ya kukuchuna tu.Hapa kwa namna yeyote ile lazima Mungu atakuadhibu tu.Utakuwa chini zaidi ya pale ulipoanzia.Utakuwa ni wakujifungia ndani tu kwani dunia yote itakuwa inakucheka wewe.Kifupi utakuwa HOHEHAHE!
Utaona aibu kwenda kumuangukia mkeo kwani nae atakuwa anaendelea na maisha yake tena kwa mafanikio makubwa kwani hakukukosea kitu.
Tubadilike kwani majuto huwa ni mjukuu!

Asante mdau uliyetuletea kero hii.

Kama una kero yeyote tuandikie kupitia rainbowinfom@gmail.com

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...