- Mtu ameandika “Sleeping” , sasa leo siku ya tano, si kishakufa huyu?
- Mwingine kaandika “Driving” toka mwaka jana Agosti, naona atakuwa anakaribia Afghanistan saa hizi
- Haya jamaa najua kalazwa anaumwa lakini kaandika “Happy” we vipi ndugu yangu?
- Huyu mdada kaandika “Available”. Sijui anajua maana yake? Tukikuibukia utaanza mitusi
- Mbosi huyu hajabadilisha status mwaka wa pili sasa, “Hey there! I’m using
- Superstar wetu mmoja kaandika “Urgent calls only”. We vipi? Kwani we faya, au ambulens au polisi?
- Haka kabishoo kameandika “Can’t talk, WhatsApp only”. Sasa una simu ya nini? Si uitupe uwe unashinda Facebook? Simu kazi yake ya kwanza kuongea sio Whatsapp, pambafu we.
- Huyu mshamba kaandika “At the movies” wiki ya saba sasa, sinema gani ndefu hivyo wewe? Au unafanya kazi ya kuuza tiketi hapo sinema?
- Dogo kaandika “At school” sasa Whatsapp ya nini? Utapata Div O wewe
- Mwezi wa pili sasa mchepuko umeandika “Busy” hivi busy unafanya nini? Nikiacha kukutumia credit utaanza kelele
- Hahahahahaha eti “Battery about to die” miezi sita mfululizo, badilisha hiyo betri? Au mtaa wenu hakuna umeme miezi sita hujachaji simu? Si kalalamikeni TANESCO? Au nikununulie jenereta? Unaudhi
- Hivi najiuliza we mdada huu mwezi wa nne sasa eti “At the gym” unajitayarisha kwa Olympic
- Bosi status yako ya “In a meeting” mwezi mzima inachekesha, maliza huo mkutano rudi kwenu. Kubwa zima jinga
CHANZO: John kitime
No comments:
Post a Comment