Vipimo
2 kikombe Mchele
1 1/2 kikombeTui la
nazi
1 KJ Mafuta
2 kjc Hamira
1 KJ Unga wa
ngano
Hiliki-Kulingana na matakwa
yako
FANYA HIVI
1· Osha na roweka mchele
usiku mzima ndani ya maji baridi.
2· Mimina vifaa
vyote isipokuwa sukari , ndani ya mashine ya kusagia (blender) na usage mpaka
mchele uwe laini.
3· Mimina ndani ya
bakuli na ufunike.Weka mahali penye joto ili mchanganyiko ufure.
4· Ukishafura ,
mimina sukari na changanya vizuri.Ongeza maziwa kidogo kama mchanganyiko ni
mzito.
5· Weka chuma
kipate moto.
6· Paka
mafuta au samli kidogo kwenye chuma kisha mimina mchanganyiko kiasi
kuunda duara na ufunike.
7· Utazame
ikishaiva upande mmoja , geuza upande wa pili mpaka iwe tayari.
8· Endelea Mpaka umalize mchanganyiko
wote; panga kwenye sahani na tayari kuliwa.
No comments:
Post a Comment