Leo tuzungumzie swala la mtu
kujiona unajua kila kitu. Ikumbukwe
maisha ni safari na vilevile ni darasa. Hata uwe na elimu gani huwezi kujua
kila kitu hivyo inatakiwa uwe na utayari wa kujifunza kila siku. Ukiangalia
wengi kati ya watu waliofanikiwa kimaisha wamekuwa na utayari wa kujifunza. Na
wale wasiotaka kujifunza kwa kuona kuwa wanajua kila kitu huwa hawaendi popote
ki maisha.
Mfano,unaweza
ikiwa unajua kupika wali wa mbogamboga, akatokea mpishi mwingine na kukuambia
kuwa yeye angependa kwa siku hiyo kutengeneza hicho chakula, Kwa mtu muungwana
na anaependa kuongeza kitu kingine kichwani mwake atamkubalia mara moja. Ila
kwa wale wenzangu na mimi wasiotaka kuonekana kuwa hawajui atakataa kuwa yeye
anajua kutengeneza wali huo wa mboga.
Hili
ni kosa kubwa sana.Kwani utakuwa umekosa nafasi adimu ya kuongeza ujuzi.
Ukitaka
maendeleo kubali kukosolewa. Hii ndiyo siri kubwa ya mafanikio.Huwezi kuwa
unajua kila kitu-HAIWEZEKANI.
Na
kama unajua kitu vilevile usiwe mchoyo kuwapa ujuzi wako watu wengine. Kwani
maisha ni kutoa na kupokea.
MWENYE MASIKIO NA ASIKIE
No comments:
Post a Comment