Thursday, 8 October 2015

KERO:ROHO MBAYA HULETA UMASIKINI NA MIKOSI




Wengi wetu huwa tunashangaa kwanini tunakuwa na maisha mabaya.Wengi husema Mungu ndiye kawapangia kuwa na maisha hayo , si kweli.Mungu hapendi kiumbe wake apate shida.Yeye hutaka tutende mema ili tulipwe mema.Moja wapo ya mema hayo ni kuwa na maisha mazuri.Nikisema maisha mazuri ina maana kuwa na shughuli yeyote ya kukupa kipato wewe mwenyewe na si kuwa tegemezi.Kipato kitakuwezesha kuwa na makazi, kujinunulia mavazi, chakula n.k
Vilevile tusisahau kumrudishia yeye aliyetujalia kuwa na uhakika wa maisha yetu kwa kutoa sadaka.


Kuna usemi usemao MALIPO YA MWOVU NI HAPA DUNIANI . Hii ni kweli kabisa.Kuna wengi wetu huficha tabia zetu halisi tulizo nazo.Mbele za watu hujifanya ni watu wema sana lakini nyuma ya pazia ni nyoka.
Huwa tunajisahau kuwa unaweza kudanganya binadamu lakini si Mungu. MUNGU HADANGANYWI.
Unapomfanyia mtu aliyekutendea mema  kitu kibaya Mungu si kipofu.Huleta majibu na huwezi kujificha .Dunia yote( kwa maana ya watu wanaokuzunguka) watakuona na hakuna wa kukusaidia.
Unaweza kupoteza kila ulichonacho na USIKIPATE TENA. Utakuwa ni mtu wa kuchekwa. Kutokana na dhamira mbovu uliyokuwa nayo na kusahau kama kuna Mungu utasema UMELOGWA kumbe mchawi wa maisha yako ni wewe mwenyewe.
Wengi wetu tumeacha maisha yetu yaongozwe na ndugu.Hapa ndiyo tunatenda kosa kubwa sana.Ukiangalia maisha ya huyo/hao ndugu wenyewe wanaokuongoza hayaeleweki. Je, iweje leo wakuongoze wewe? Wengi hufanya hivi wakitaka kukutumia kwa manufaa yao na wala si kwamba wanajali maisha yako wewe, Kama wangekuwa wanajali maisha yako wangekushauri katika vitu vya maendeleo ila wanajua kwa kufanya hivyo utajali vitegauchumi vyako na wao watakosa kwa kuponea.Wataanza kukushauri vitu vibaya na hapa ndiyo swala la roho mbaya linapojitokeza. Kwa njaa zao watakufanya na wewe uwe na roho mbaya kama zao na mwisho wa yote ni kuwatendea mabaya wale waliowatendea mema. MUNGU HATAWAACHA. Laana ya Mungu ni mbaya. Haitoki mpaka ukaombe msamaha hadharani kwa kukiri yale yote mabaya uliyoyafanya ikiwemo.
Mtateseka mpaka mnaingia kaburini.
Ila wale mliowalipa mabaya MUNGU ATAWANYANYUA. Mtawakimbia kwa aibu kutokana na ubaya mliowafanyia na mabaya mliyowazushia.
Mwenye masikio na asikie

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...