Kuna hili tatizo la ndugu wa mume
kuingilia ndoa ya ndugu yao.Hii inahusu sana mawifi ambao wengi wao huwa ndiyo
chanzo cha ndoa nyingi kuvunjika.Na wengi hufanya hivi kwa maslahi yao binafsi
na wala si kwa maslahi ya kaka zao. Ukichunguza wengi ya mawifi hawa ni
umaskini na roho mbaya tu ndiyo huwa vinawasumbua. Ili watimize uovu wao
hutafuta visingizio na hadithi nyingi za kutunga kuonyesha uovu wa wifi wasiyemtaka wanaweza kusingizia kuwa wifi
yao ni mshirikina n.k. Hakuna kitu kibaya duniani kama kusingizia mtu mambo
yasiyokuwa kweli kwani malipo yake huja
vibaya. Vitabu vya dini vinakataza kumsingizia jirani yako uwongo, hivyo muwe
makini kwani uwongo huenda ukawaponza.
Hapohapo wengine humtafutia kaka
yao mwanamke ambaye wao wanatumaini kuwa watakuwa na manufaa nae. Ila huwa
hawajui kuwa wanaweza kupoteza kipande
cha almasi na kuokota kipande cha chupa! Kuna kitabu cha hadithi kilichoandikwa
na Hammie Rajabu kiitwacho “Gubu la Wifi”.
Katika kitabu hiki mawifi wawili
walimchukia wifi yao bila sababu yeyote. Wifi yao aliwapenda sana na
aliwafanyia mengi mema.Wao hawakujali hayo bali walikuwa wana mwanamke
waliyempenda wao ambaye ndiye walitaka awe wifi yao. Walimfanyia wifi yao vitimbi vyote na kuanza kumpika kaka
yao kwa uwongo mpaka nae akaiva. Mwishoni akamwacha mkewe.
Akaolewa waliemtaka. Unajua nini
kilitokea?Walilotegemea siyo lililotokea.Wifi mpya hakutaka kuwaona kabisa
nyumbani kwake.Ni yeye ndiye aliwanyanyasa
mpaka wakamkumbuka wifi yao wa kwanza ambae alikuwa na upendo sana nao. Wifi
wa kwanza akaolewa tena na mume mwenye nafasi yake nzuri kimaisha zaidi ya mume
wa kwanza.
Jamani mawifi acheni roho
mbaya.Kama mmeshindwa na maisha yenu msiharibu maisha ya watu wengine.Mungu
hapendi sababu kusononeka kwa mke aliyeachwa kutawafanya nyie maisha yenu
yapoteze mwelekeo kabisa.
MWENYE MASIKIO NA ASIKIE!
No comments:
Post a Comment