Skip to main content

Posts

Showing posts from November, 2013

BALOZI WA COCA COLA DAVID CORREY ATUA DAR NA KOMBE LA DUNIA, MAMIA WAFURIKA KULIONA

Balozi wa FIFA Coca-Cola David Correy kutoka Marekani aliyeimba wimbo rasmi wa Brazil World Cup 2014  akiongea na waandishi wa habari kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo ambapo maelfu ya Watanzania wamepata fursa ya kushuhudia kombe halisi la FIFA la Dunia na kupiga nalo picha kwa karibu.

MWANAMUZIKI MKONGWE WA CONGO, TABU LEY ROCHEREAU AFARIKI DUNIA

Mwanamuziki mkongwe wa Congo, Pascal Tabu Ley Rochereau amefariki dunia leo asubuhi baada ya kulazwa katika hospitali ya nchini Ubelgiji.

Kwa mujibu wa mwanae Charles Tabu, aliyeongea na Radio Okapi, Tabu Ley amefariki kwa kiharusi na Kisukari. Naye Nyboma Mwandido, mwanamuziki mwenzie aishiye jijini Paris, Ufaransa amethibitisha kifo cha msanii huyo kilichotokea leo Jumamosi saa 2 asubuhi Brussels. Tabu Ley alikuwa mgonjwa mahututi kwenye hospitali hiyo kutokana na kusumbuliwa na kiharusi alichokipata mwaka 2008.

Tabu Ley akishirikiana na Sam Mangwana kuimba kibao maarufu "Afrika mokili mobimba"

AFRICAN PRINT DESIGNS

LACE WIGS ZA AINA TOFAUTI

USHAHIDI WA UMILIKI WA ZIWA NYASA WATOLEWA

Watu wa viunga vinavyolizunguka Ziwa Nyasa /Ziwa Malawi wakiendelea na shughuli za uvuvi. Tafiti mbalimbali zimeonyesha wengi wao hawaelewi hasa chanzo cha mtafaruku huu wa mipaka ya Ziwa ulioibuka kati ya Tanzania na Malawi. PICHA | PLATOURS (KWA HISANI)  Dar es Salaam. Malawi na Tanzania zimewasilisha ushahidi na majibu ya maswali kuhusu umiliki wa maeneo kwenye Ziwa Nyasa, kwa jopo la wasuluhishi linaloongozwa na Rais mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano. Wasuluhishi hao walizitaka Malawi na Tanzania kutoa majibu ya maswali manne muhimu, wakati wakiwasilisha ushahidi wao kuhusu umiliki wa ziwa hilo wenye mgogoro. Mgogoro huo uliibuka baada ya Serikali ya Malawi bila kushauriana na Tanzania kutoa leseni kwa kampuni mbili za kigeni, kutafuta mafuta katika eneo la ziwa ambalo linamilikiwa na Tanzania. Kwa mujibu wa gazeti la mtandaoni la Malawi la  Nyasa Times, msemaji wa Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa Malawi, Quent Kalichero alithibitisha Jumatano wiki hii kwamba nchi…

Shahidi aeleza Twiga walivyokuwa wanakamatwa

Joto la mishahara: ‘Viongozi utendaji dhaifu, kipato kikubwa’

Rais Jakaya Kikwete alinukuliwa katika kikao cha OGP London akisema mishahara ya viongozi wa umma haiwezi kuwa siri kwani ni sehemu ya bajeti, ingawa leo hii wengi katika serikali yake wanatetea usiri uliokithiri katika suala zima la vipato vya ‘wakubwa.’ PICHA | MAKTABA Dar es Salaam. Ripoti mpya ya utafiti imebainisha kuwa mishahara mikubwa wanayolipwa viongozi wa juu serikalini na wanasiasa hailingani na utendaji wao wa kazi. Ripoti hiyo iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam, imeeleza kuwa viongozi hao wanalipwa mishahara inayotofautiana kwa kiwango kikubwa na pato la mwananchi wa kawaida. Huku ikitaja mapato ya mishahara ya marais wa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ikiwamo Tanzania, imesema kuwa hali hiyo ni kuibebesha jamii mzigo wa kugharimia malipo ya viongozi.

KATUNI YA LEO

RAIS JK AAGIZA KUKAMATWA KWA WANAOOA WANAFUNZI-HONGERA RAIS KWA KUTEGUA KITENDAWILI HIKI!

Rais Jakaya Kikwete, ameviagiza vyombo vya dola na viongozi wa ngazi mbalimbali nchini, kuanza mara moja kufanya msako mkali wa kuwakamata watu wanaoa wanafunzi wa kike wa shule za msingi na baada ya kukamatwa wafikishwe katika vyombo vya sheria kwa makosa ya ubakaji.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZIKO YA MTOTO WA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM, PETER MANGULA MAKABURI YA KINONDONI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka udongo katika kaburi la mtoto wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, (Peter Mangula), wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika katika makaburi ya Kinondoni Kisutu jijini Dar es Salaam,leo. Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, akiweka udongo kwenye kaburi la mtoto wake, Peter Mangula, wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika katika makaburi ya Kinondoni Kisutu jijini Dar es Salaam,leo.


 Watoto wa marehemu, wakiweka udongo kwenye kaburi ikiwa ni ishara ya kumzika baba yao.
Kwa picha zaidi bofya "READ MORE"

RAIS KIKWETE APOKEA KOMBE LA DUNIA

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akilifunua Kombe la Dunia katika uwanja wa michezo Kirumba mjini Mwanza leo jioni. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akianza kulinyanyua Kombe la Dunia katika uwanja wa michezo Kirumba mjini Mwanza leo jioni. Kombe hilo limerejea jijini Dar es Salaam na kesho wananchi watapata fursa ya kupiganalo picha

AINA FOFAUTI ZA WIGI KWA WANAWAKE

PICHA: MABADILIKO YA MSIMU ULAYA

Picha mbili juu zinaonyesha jinsi miti ilivyokuwa  ikionekana majira ya autumn
Picha hii ikionyesha miti hiyo inavyoonekana sasa(winter)

TANGA SASA HATARINI KUPOTEZA HADHI YA JIJI

Halmashauri  ya Jiji la Tanga inaweza kushushwa hadhi kuwa manispaa kutokana na kushindwa kukusanya mapato.
Hayo yalibainishwa jana na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) wakati wa majumuisho ya ziara yao.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Rajabu Mbaruk, alisema kamati inakwenda kuishauri serikali kushusha hadhi ya kuwa jiji na kurudi katika hadhi ya manispaa kwa kuwa imeshindwa kukusanya mapato.

Dawa za Kulevya: ‘Afrika Kusini sasa tishio kwa vijana’

“Tarehe 26 hadi 31 ya Oktoba nilikuwa kwenye mkutano huko Afrika Kusini  na Jeshi la Polisi la nchi hiyo, lilitoa taarifa kuwa kuna ongezeko kubwa la viwanda vinavyotengeneza dawa za kulevya ndiyo maana vijana wengi wanatumika ama kupeleka kemikali au kusafirisha dawa hizo kwenda katika nchi nyingine,” Alfred Nzowa Wakati watanzania  wawili waliokamatwa na kilo 55 za dawa za kulevya huko Erhukuleni, Ghauteng, Afrika Kusini, wakipanda kizimbani leo, Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya,Alfred Nzowa, amesema, nchi hiyo sasa ni tishio. Alisema Watanzania wengi wameingia katika biashara ya dawa za kulevya kwa sababu ya viwanda vya kutengeneza dawa hizo, vilivyoenea katika sehemu nyingi za nchi hiyo.  Kamishna Nzowa alisema hivi sasa nchi hiyo ina viwanda vya kutengeneza dawa za kulevya ndiyo maana hata Julai mwaka huu, Watanzania wawili, Agnes Gerald na Melisa Edward walikamatwa wakiwa na kemikali za kutengeneza dawa hizo, zifahamikazo kama Ephedrine.

AFRICAN PRINT

AFRICAN PRINT KWA WANAUME

KATUNI YA LEO

PICHA NA MALEZO JUU YA BRASHI ZA MAKE UP NA UTUMIAJI WAKE

LAMPSHADES ZINAWEZA KUPENDEZESHA NUMBA YAKO

KWA WAPENDA RABA ANGALIA AINA ZA CONVERSE -ALL STAR

KAPTENI MSTAAFU ROBERT: SITASAHAU NILIPOHUKUMIWA MAISHA JELA -SEHEMI YA 2

Rubani wa ndege aliyeonja kifo kwa ajali ya ndege na kifungo cha maisha,  Rubani huyu ni Kapteni Mstaafu Rodrick Robert(69). Picha na Maktaba  Mwandishi: Unakumbuka nini kwenye vita hivyo? Rubani: Nakumbuka siku moja nilikuwa off (napumzika kidogo), nikaamua kunywa bia. Na ratiba ilikuwa ikionyesha nitakuwa kazini kesho yake. Lakini ghafla kiongozi wangu alinijia na kunitaka nirushe ndege. Mimi nilikataa katakata kwa sababu nilikuwa nimekunywa pombe. Niliwahi kumwendesha Nyerere. Mwandishi: Je, ni kweli ulimwendesha Nyerere? Na kazi ya jeshi iliendelea hadi lini? Rubani: Ni kweli baada ya vita vya Amini niliendelea kurusha ndege za jeshi na pia kufanya kazi ya kuendesha ndege ya Rais Nyerere. Mwaka 1983 Januari 7, nilikamatwa na wanajeshi wengine wengi kwa tuhuma za uhaini. Tulidaiwa tulitaka kumuua Rais Julius Nyerere.

MAJANGA MENGINE HAYA: MTOTO WA MIAKA 8 AAJIRIWA KUWA MFANYAKAZI WA NDANI

Hivi huyu mtu anayeajiri mtoto wa miaka 8 ana akili sawa kweli? Hivi anaweza kumtoa mwanae wa kumzaa mwenye umri huu kwenda kufanyishwa kazi? Kwanini tunakuwa na mioyo ya kikatili kiasi hiki?Hii habari imenisikitisha sana.Ningemwelewa huyu mwanamke kama angalimchukua huyu mtoto na kumsomesha huku akimtunza kama anavyotunza watoto wake. Masikini,mtoto anaelezea moja wapo ya majukumu yake ni kumtunza mtoto na kufua.Hivi kwa umri huu ana uwezo wa kuangalia mtoto ? Yeye mwenyewe ni mtoto anayehitaji kutunzwa. Hivi mtoto huyu atafua nguo zikatakata?Huyu mwanamke aliyefanya hivi hastahili kuwa mama.
Pongezi kwako Joyce Kiria kwani bila wewe kupitia kipindi chako"WANAWAKE LIVE" tusingeweza kufahamu hili pamoja  na matatizo mengine yalimo ndani ya jamii yetu.Endeleza kazi nzuri ili tuokoe wanawake wenzetu na watoto wetu.

KAPTENI MSTAAFU ROBERT: SITASAHAU NILIPOHUKUMIWA MAISHA JELA -SEHEMI YA 1

Rubani wa ndege aliyeonja kifo kwa ajali ya ndege na kifungo cha maisha, Rubani huyu ni Kapteni Mstaafu Rodrick Robert(69). Picha na Maktaba

Nje kidogo ya Mji wa Songea, kipo kijiji kinachoitwa Mateka. Bila shaka jina la kijiji hicho lina historia yake, lakini kubwa ni kwamba ndiko anakoishi rubani wa ndege aliyeonja kifo kwa ajali ya ndege na kifungo cha maisha. Rubani huyu ni Kapteni Mstaafu Rodrick Robert (69) mrefu, mweupe ambaye si mnene na wala si mwembamba akiwa na nywele laini zinazoashiria wazi kwamba mmoja wa wazazi wake alikuwa mtu wa nje ya Bara la Afrika.

Tuhuma zang’oa maofisa Maliasili

Waziri wa Maliasili ya Utalii, Balozi Khamisi Kagasheki akifungua mkutano wa wadau wa wanyamapori Dar es Salaam, jana. Picha na Emmanuel Herman

Dar es Salaam. Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki amesema wizara yake imewasimamisha kazi baadhi ya maofisa kutokana na kujihusisha na biashara haramu ya ujangili wa meno ya tembo. Akizungumza baada ya kufungua warsha ya wadau wa wanyamapori jana, Balozi Kagasheki alisema mapambano dhidi ya ujangili yanakabiliwa na changamoto nyingi kutokana na kuhusisha mtandao mkubwa ambao ndani yake kuna watu wazito na vigogo serikalini. “Biashara hii wacha bwana, ni ngumu kwelikweli, inahusisha mtandao mkubwa… tayari tumewasimamisha baadhi ya watumishi na hivi karibuni nitayaweka wazi majina ya vigogo na watu wengine wanaojihusisha na mtandao huu.

EXCLUSIVE: SIRI 5 ZA WOLPER ZAVUJA

Na Sifael Paul
MOYO huhifadhi mengi mazito hasa ya kuumiza! Staa mkubwa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amejikuta akimwaga machozi wakati akianika siri tano nzito kuhusu mapenzi katika mahojiano (exclusive interview) na Amani kwa takriban saa mbili. Wolper akifunguka ndani ya Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar. Katika ‘intavyu’ hiyo iliyofanyika Jumatatu iliyopita kwenye Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar kuanzia saa 8:44 alasiri hadi saa 10:44 jioni, Wolper alifunguka vitu vingi. KISA/MKASA
Akizungumza kwa masikitiko, uchungu na majuto, Wolper alisema hawezi kumsahau mwanaume huyo ambaye ni Abdallah Mtoro ‘Dallas’ kwa namna alivyomwingia kijanja na kutaka kumvunjia heshima aliyoijenga karibia miaka kumi nyuma.

MAMBO YA NAIJA HAYO. ASO EBI!

VIATU KUTOKA KWA MBUNIFU CHRISTIAN LOUBOUTIN (CL)