Kuni ambayo hutumika kama nishati ya kupikia hufuatwa mbali na kwa wengi wao hili ni zoezi la kudumu |
Hawa wamebahatika kuwa na maji jirani |
Ukamuaji wa maziwa ni moja ya kazi za wakina mama katika jamii nyingi |
Wanawake wengi hutembea umbali mrefu kupata mahitahi mbalimbali ya familia |
Kutokuwepo uhakika wa maji hufanya wanawake wengi kufuata maji mbali |
Baadhi ya wanawake wameelemewa na mzigo wa kazi za nyumbani zikiwemo kupika,usafi, kuchota maji na kutafuta kuni pamoja na kulima na kujitafutia kipato. Wanawake wenye wakati mgumu sana ni wale wa kijijini na ambao ndiyo wengi.
Kitakachoweza kumkomboa mwanamke ni ELIMU.
Faida ya elimu kwa wanawake ipo katika nyanja zote katika jamii. Mbali na kuchangia kwenye uchumi wa taifa, wanawake wenye elimu ni muhimu katika sekta binafsi kwani wengi wao huweza kujiajiri wenyewe na kuacha kuwa tegemezi kwa waume zao.
Elimu kwa wanawake pia kuhusishwa na ongezeko katika pato la familia,afya na lishe bora, uangalizi mzuri wa watoto, n.k
Wanawake walioelimika huchelewa kuolewa na huzaa watoto wachache.
Kwa kila mwaka wa elimu kwa mwanamke hupunguza asilimia 7-9 ya vifo vya watoto.
Je,wanawake wanaweza kufanyanini ili kuboresha kipato?Tukutane katika muendelezo wa makala hii.
No comments:
Post a Comment