Washindi wa kwanza wa nusu fainali ya kwanza ya Guiness Football Challengekutoka Ghana Naab Jonathan Baan(kushoto) na Desmond Odaano(kulia) katika picha ya pamoja na waendeshaji wa kipindi cha Pan-Africa Guinness Football Challenge Larry Asego na Mimi Kalinda.
Mei 23 2013, Dar es Salaam: Jana usiku kupitia televisheni za ITV na Clouds TV nusu fainali ya kwanza kabisa ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ ilirushwa hewani na katika runinga Afrika nzima ambapo timu ya Ghana ilionesha ni kwanini ni timu bora ambayo ndiyo imejishindia pesa nyingi mpaka sasa.
Jonathan Nabb na Desmond Odaano walionesha uwezo na ujasiri wao walipoibuka washindi zidi ya wapinzani wao timu kutoka Kenya katika mchezo wa jana.
Katika hatua ya pesa ukutani walifanikiwa kulenga lango namba nne na hivyo kupata dola za kimarekani 12,000 wanazoziongeza katika dola 8,500 walizokuwa nazo awali katika hatua ya robo fainali.
Wakenya Francis Ngigi na Kepha Kimani ambao ni washindi wa pili katika nusu fainali hii wataungana na Ghana katika fainali. Ingawa waliikosakosa hatua ya ukuta wa pesa wa Guinness bado wana nafasi ya kuwa mabingwa katika fainali.
No comments:
Post a Comment